Friday, January 27, 2012

Mabibi na Mabwana,
Ninasikitika kuwa kutokana na kamera/Simu yangu kuibiwa na vibaka wa Bongoland, nimesitisha kuweka picha mpya kwenye blog hii kwa muda.
Na kutokana na haya 'Maisha Magumu kwa Kila Mtanzania' yaliyoshika kasi ukiachilia mbali mimi kuwa Mstaafu, huenda hali hii ya kutokuwepo na picha mpya kwenye Blog yetu hii ikachukua muda kidogo. Tusameheane na Tuvumiliane...!

Wednesday, May 11, 2011


Mambo ya kisasa yanaenda yakiongezeka! Kiwanda kipya na cha kisasa cha uchapaji magazeti, vitabu, majarida, vipeperushi, madaftari na kadhalika kilichofunguliwa hivi karibuni huko Mapia, Bagamoyo.
Posted by Picasa

Biashara Matangazo! Kwa hisani ya Michuzi Blog
Posted by Picasa
Posted by Picasa

Wiki hii huku Mbezi kwetu tumeamka na Ukungu huu. Umenikumbusha sana kwetu Usambaani!
Posted by Picasa

Saturday, January 08, 2011


Michael Owen wa Manchester United wa Mbezi mwisho akivua samaki kwenye Mtaro wa maji machafu eneo la Mbezi Shamba

Posted by Picasa

Monday, December 27, 2010


Siku hizi kwenda kwetu ni Starehe! Mabasi kama Ndege vile! Twaja lheo twaondoka lheo lheo!
Posted by Picasa

Hapa ndio Jikoni penyewe katika masuala ya mawasiliano. Si haba.
Posted by Picasa

Kweli Mchina kaleta mambo!
Posted by Picasa

Safari ya kupeleka Bidhaa mikoani usiku wa kuamkia sikukuu ya Krisimasi imeishia Mbezi kwa Yusufu kwenye Mtaro!
Posted by Picasa

Tuesday, December 01, 2009


Mtaa wetu sasa Unapendeza, Asante Voda!
Posted by Picasa

Kila mahali, Watu Kibao...hasa kwenye ATM!
Posted by Picasa

Kwa wale ambao hawali sana mchicha, kwenye tangazo hili lililopo nje ya moja za ofisi zake Halimashauri ya manispaa ya Temeke inatuambia kuwa imedhamiri kuwa wakazi wote wa Manispaa; Wanawake kwa Wanaume wawe wameondokana na umasikini, wamepata Elimu, wanaishi katika maisha bora kwenye makazi na miundombinu bora chini ya Uongozi wa Kidemokrasia unaozingatia maadili ya Utawala bora na kuheshimu Umoja wa Kitaifa ifikapo.......2010 yaani Mwaka Kesho!
Posted by Picasa

Makazi ya baadhi ya Wakazi wa eneo la Jangwani.
Posted by Picasa


Shortcut yetu ya Jangwani kutoka Kariakoo kwenda Kigogo. Inategemewa kupunguza foleni kubwa wakati wa asubuhi na jioni kwenye barabara ya Morogoro.
Posted by Picasa