Milima Ya Kwetu : Mombo
Mtaa wetu sasa Unapendeza, Asante Voda!
Kila mahali, Watu Kibao...hasa kwenye ATM!
Kwa wale ambao hawali sana mchicha, kwenye tangazo hili lililopo nje ya moja za ofisi zake Halimashauri ya manispaa ya Temeke inatuambia kuwa imedhamiri kuwa wakazi wote wa Manispaa; Wanawake kwa Wanaume wawe wameondokana na umasikini, wamepata Elimu, wanaishi katika maisha bora kwenye makazi na miundombinu bora chini ya Uongozi wa Kidemokrasia unaozingatia maadili ya Utawala bora na kuheshimu Umoja wa Kitaifa ifikapo.......2010 yaani Mwaka Kesho!
Makazi ya baadhi ya Wakazi wa eneo la Jangwani.
Shortcut yetu ya Jangwani kutoka Kariakoo kwenda Kigogo. Inategemewa kupunguza foleni kubwa wakati wa asubuhi na jioni kwenye barabara ya Morogoro.
Kikombe cha Chai na 'Kisahani' chake - Korogwe
kila mahali....Watu Kibao!!
Madini ni ya kwetu, Kwa nini tusiyape jina la 'Kiswahili'??

Enzi hizo ukiona 'Mtemba' kama huu unaondoka Bandari ya Salama basi unajua kabisa kuwa panga pangua humo ndani hamkosi vijana wetu wawili watatu wamedandia kwenda kutafuta maisha Ulaya! Siku hizi sina hakika hata kama wanajua neno 'Mtemba'!
Wabongo! Labda tujaribu kuandika kinyume ndio watu wataelewa! Ukitaka watu wasitupe takataka mahali basi wewe andika 'Ni RUHUSA KUTUPA TAKATAKA HAPA'!
Kwa hadhi yake na eneo iliyopo, tunategemea wazee wetu wa Mpira waingie mikataba na wazee wa ujenzi kama NSSF na NPF (Nasikia ni mashirika ya Akiba za Wafanyakazi!) ili watujengee 'Kitu' chenye hadhi zaidi ya hiki!
Tairi limechomoka. Mwisho wa safari. Marejesho ya Nauli!
Uongo mbaya, Bongo siku hizi mambo sio mabaya sana kwenye suala la kujenga 'Vibanda'...!
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Moshi, Muuza Duka mmoja Mbunifu alichoka kuibiwa vitu vyake na kuamua kumnyoa Mbwa wake kwa staili ya Simba Shave! Taarifa ni kwamba hakuna Kibaka anayesogelea Duka hilo sasa Hivi! Habari/Picha kwa hisani ya Blog ya Brother Adam Lusekelo.
Michael Jackson ...Alikuja...Akaona...Akatawala Ulimwengu wa Muziki...Ameondoka.
Baada ya kutimuliwa Jangwani, ambapo pia yameisharudi tena, magari makubwa yamevamia mitaa yetu ya uswahilini na kufanya ndio Parking zao!
Wakati Waya unaopita chini ya bahari wa Fibre Optic unategemewa kurahisisha mawasiliano ya Internet kwa kiasi kikubwa, Mchoraji Gado ana wasiwasi....!
Picha/Kibonzo kwa Hisani ya Gado.