Hili ndio Soko Kuu la Bumbuli ambalo liko eneo la Salem na
huwa siku ya Jumanne na Jumamosi. Picha hii imepigwa siku
ya Jumapili mchana ambapo wenyeji wa eneo hilo wanakuwa
majumbani wakipumzika. Nyuma ni eneo la Mlima wa Kwentui
ambao ni maarufu sana kwa Picnic siku za Sikukuu na Ubarikio.