Sunday, February 22, 2009

Hili ndio Soko Kuu la Bumbuli ambalo liko eneo la Salem na
huwa siku ya Jumanne na Jumamosi. Picha hii imepigwa siku
ya Jumapili mchana ambapo wenyeji wa eneo hilo wanakuwa
majumbani wakipumzika. Nyuma ni eneo la Mlima wa Kwentui
ambao ni maarufu sana kwa Picnic siku za Sikukuu na Ubarikio.

MADUDA: Hii ni shule mashuhuri sana 'Bumbuli City' ambayo
Wasomi wote wa miaka ya 50 hadi 70 wa 'jiji' hilo walisoma hapo
wakati huo ikijulikana kama 'Maduda Upper Primary School'
ikiwa na madarasa kutoka la Tano hadi la Saba.
Sasa hivi ni Shule ya Sekondari.