Enzi hizo ukiona 'Mtemba' kama huu unaondoka Bandari ya Salama basi unajua kabisa kuwa panga pangua humo ndani hamkosi vijana wetu wawili watatu wamedandia kwenda kutafuta maisha Ulaya! Siku hizi sina hakika hata kama wanajua neno 'Mtemba'!
Wabongo! Labda tujaribu kuandika kinyume ndio watu wataelewa! Ukitaka watu wasitupe takataka mahali basi wewe andika 'Ni RUHUSA KUTUPA TAKATAKA HAPA'!
Kwa hadhi yake na eneo iliyopo, tunategemea wazee wetu wa Mpira waingie mikataba na wazee wa ujenzi kama NSSF na NPF (Nasikia ni mashirika ya Akiba za Wafanyakazi!) ili watujengee 'Kitu' chenye hadhi zaidi ya hiki!
Tairi limechomoka. Mwisho wa safari. Marejesho ya Nauli!
Uongo mbaya, Bongo siku hizi mambo sio mabaya sana kwenye suala la kujenga 'Vibanda'...!
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Moshi, Muuza Duka mmoja Mbunifu alichoka kuibiwa vitu vyake na kuamua kumnyoa Mbwa wake kwa staili ya Simba Shave! Taarifa ni kwamba hakuna Kibaka anayesogelea Duka hilo sasa Hivi! Habari/Picha kwa hisani ya Blog ya Brother Adam Lusekelo.
Michael Jackson ...Alikuja...Akaona...Akatawala Ulimwengu wa Muziki...Ameondoka.
Baada ya kutimuliwa Jangwani, ambapo pia yameisharudi tena, magari makubwa yamevamia mitaa yetu ya uswahilini na kufanya ndio Parking zao!