Wadau wakiwa kwenye matembezi ya Jumapili jioni. Nyuma yao ni jengo la hoteli ya HOLIDAY INN ambayo kuanzia tarehe Moja Juni inabadilishwa jina na kujulikana kama SOUTHERN SUN. Kuna siri gani katika huu ubadilishaji wa majina ya mahoteli yetu kila baada ya 'siku mbili tatu'???
Milima ya Kwetu. Nje ya eneo la mapokezi ya Wagonjwa, OPD, la Hospitali ya Bumbuli Mission unakutana na View hii. Ni lazima utaanza kujisikia nafuu hata kabla hujaanza matibabu! Chini ni mabweni ya Chuo Cha Waganga Bumbuli MATC.
Bumbuli Mission Hospital na Chuo cha Waganga Bumbuli MATC, kushoto, iliyojengwa na wamisionari kutoka Ujerumani mwanzoni mwa miaka ya 60 ni miongoni mwa vivutio vinavyofanya kijiji cha Bumbuli kufahamika kama Bumbuli City!