Tuesday, May 20, 2008


Wadau wakiwa kwenye matembezi ya Jumapili jioni. Nyuma yao ni jengo la hoteli ya HOLIDAY INN ambayo kuanzia tarehe Moja Juni inabadilishwa jina na kujulikana kama SOUTHERN SUN. Kuna siri gani katika huu ubadilishaji wa majina ya mahoteli yetu kila baada ya 'siku mbili tatu'???
Posted by Picasa

3 comments:

Anonymous said...

Wizi tu kaka unadhani nini?

Anonymous said...

Hakuna wizi wowote, ni kutofahamu kwenu.
Waendeshaji wengi wa mahoteli huwa sio wamiliki wa miradi au majengo ya miradi husika. Wamiliki hukabidhi miradi na kuwekeana mikataba ya uendeshaji na wataalamu wa uongozaji wa miradi ya hoteli kwa kipindi maalumu kilichokubaliwa kwa pamoja kati ya pande hizo mbili. Waendesha miradi hulazimika kulipa faida kwa wamiliki wakiwa wametoa makato ya kiwango cha asilmia (percentage) waliyokubaliana katika mikataba yao.

Iwapo mkataba utasitishwa kwa sababu yoyote ile, mmiliki wa mradi hawezi kuendelea kutumia jila la awali la kibiashara kwani jina hili linamilikiwa na mwendeshaji kishearia. Mmiliki huwa huru wa kutafuta mwendeshaji mpya au kubuni jina lake la kibiashara iwapo atadhamiria kuendesha biashara ya hoteli.

Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa hoteli iliyokuwa ikienda kwa jina la Sheraton Dar es Salaam Hotel iliyokuwa ikiendeshwa na ITTSheraton na baadaye Starwood Hotels & Resorts Inc. ambayo mmiliki wake halisi ilikuwa TANRUSS Investments Ltd. TANRUSS iliingia mkataba wa kiuendeshaji na matapeli wa Legacy Hotels & Resorts ya Bondeni ambao haikuwachukua miaka thalatha biashara ikawashinda na wakabwaga manyanga. TANRUSS hawakuwa na ubavu wa kuiendesha lile jengo katika biashara ya mahoteli, hawakuwa na jinsi bali kuiuzilia mbali kabisa kwa waarabu, ambao nao wameingia mkataba wa uendeshaji na Muuv en piiik!

Hii ni hali ambayo tutaendelea kuiona siku zote. Iliyokuwa Kilimanjaro Hotel sasa inandeshwa na Kempinski group. Ni hali ya kawaida sana.

Lakini cha kusha&ngaza ni kuwa hata wale tunaowategemea katika kutunga et sheria hawajui hilo. Utakuta wanaropoka tu bungeni et, aah, wakwepa kodi, mara sijui nini, ... upuuzi mtupu. Mambo hayo hutokea kila nchi, na si kwa mahoteli tu. Hata hapo Bongo, angalia iliyokuwa Mobitel, baada ya kuuzwa mnategemea kuwa bado itatumia jina hilo hilo la BUZZ? Mbona hamuulizi? Hebu angaia Zain, si ni ile iliyokuwa Celtel? Wabunge wetu walioelimika hawajui hilo?

NI SWALA LA ELIMU NA UFAHAMU MDOGO TU, si vinginevyo.

Nawasilisha from Alger!
Binka

Anonymous said...

Mdau wa Algers, Tunakushukuru kwa kuongeza ufahamu wetu kwa maelezo yako mema. Tumeelewa. Bila shaka inakuwa ni bahati mbaya tu kwamba ubadilishanaji huu wa wamiliki wa miradi unafanyika baada ya miaka mitano ya nafuu ya kodi kwisha!!

Hayo ya Celtel na Zain labda ukija nyumbani ndio unaweza kutuelewesha vyema kinachoendelea pale maana hakuna ajuaye tangia pale TTCL ilipouza hisa zake bure na kuzaa Celtel!!