Tuesday, December 01, 2009


Mtaa wetu sasa Unapendeza, Asante Voda!
Posted by Picasa

Kila mahali, Watu Kibao...hasa kwenye ATM!
Posted by Picasa

Kwa wale ambao hawali sana mchicha, kwenye tangazo hili lililopo nje ya moja za ofisi zake Halimashauri ya manispaa ya Temeke inatuambia kuwa imedhamiri kuwa wakazi wote wa Manispaa; Wanawake kwa Wanaume wawe wameondokana na umasikini, wamepata Elimu, wanaishi katika maisha bora kwenye makazi na miundombinu bora chini ya Uongozi wa Kidemokrasia unaozingatia maadili ya Utawala bora na kuheshimu Umoja wa Kitaifa ifikapo.......2010 yaani Mwaka Kesho!
Posted by Picasa

Makazi ya baadhi ya Wakazi wa eneo la Jangwani.
Posted by Picasa


Shortcut yetu ya Jangwani kutoka Kariakoo kwenda Kigogo. Inategemewa kupunguza foleni kubwa wakati wa asubuhi na jioni kwenye barabara ya Morogoro.
Posted by Picasa

Saturday, August 08, 2009


Enzi hizo ukiona 'Mtemba' kama huu unaondoka Bandari ya Salama basi unajua kabisa kuwa panga pangua humo ndani hamkosi vijana wetu wawili watatu wamedandia kwenda kutafuta maisha Ulaya! Siku hizi sina hakika hata kama wanajua neno 'Mtemba'!
Posted by Picasa

Wabongo! Labda tujaribu kuandika kinyume ndio watu wataelewa! Ukitaka watu wasitupe takataka mahali basi wewe andika 'Ni RUHUSA KUTUPA TAKATAKA HAPA'!
Posted by Picasa

Thursday, August 06, 2009


Kwa hadhi yake na eneo iliyopo, tunategemea wazee wetu wa Mpira waingie mikataba na wazee wa ujenzi kama NSSF na NPF (Nasikia ni mashirika ya Akiba za Wafanyakazi!) ili watujengee 'Kitu' chenye hadhi zaidi ya hiki!
Posted by Picasa

Tairi limechomoka. Mwisho wa safari. Marejesho ya Nauli!
Posted by Picasa

Uongo mbaya, Bongo siku hizi mambo sio mabaya sana kwenye suala la kujenga 'Vibanda'...!
Posted by Picasa
Posted by Picasa

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Moshi, Muuza Duka mmoja Mbunifu alichoka kuibiwa vitu vyake na kuamua kumnyoa Mbwa wake kwa staili ya Simba Shave! Taarifa ni kwamba hakuna Kibaka anayesogelea Duka hilo sasa Hivi! Habari/Picha kwa hisani ya Blog ya Brother Adam Lusekelo.
Posted by Picasa

Michael Jackson ...Alikuja...Akaona...Akatawala Ulimwengu wa Muziki...Ameondoka.
Posted by Picasa

Baada ya kutimuliwa Jangwani, ambapo pia yameisharudi tena, magari makubwa yamevamia mitaa yetu ya uswahilini na kufanya ndio Parking zao!
Posted by Picasa

Tuesday, June 23, 2009


Wakati Waya unaopita chini ya bahari wa Fibre Optic unategemewa kurahisisha mawasiliano ya Internet kwa kiasi kikubwa, Mchoraji Gado ana wasiwasi....!

Picha/Kibonzo kwa Hisani ya Gado.
Posted by Picasa

Sunday, June 21, 2009


Fun-Runner wa Vodacom Half-Marathon akipita mtaa wa Samora huku Akilindwa na Sanamu ya Bismark!
Posted by Picasa
Vodacom Half Marathon! - Hapa Washindani wameishapita kitambo Watu wanawashangalia wale Fun-Runners!
Vodacom

Thursday, June 18, 2009


Mtaa umefungwa, pengine bila kibali kutoka mamlaka zinazohusika, turubai linaandaliwa ili shughuli ianze! Haukuwa msiba.
Posted by Picasa

Milima ya Kwetu! Mandhari ya barabara ya Mombo-Korogwe!
Posted by Picasa

Mambo ya Uswahilini! Kunapokuwa na sherehe mahali basi spika zinatundikwa kwenye nguzo za umeme! Hatari Tupu!
Posted by Picasa