chesimpilipili
kweli haya mambo bado ni mageni kwa tulio wengi. hapa nilitaka kuwawekea picha moja kuonyesha jinsi ninavyoachia mdomo wakati ninapotafuta cha kuandika. katika kuminya huku na kule, nikashitukia zimetoka mbili tena sio pale nilipotaka zitokee. maana mimi nilitaka itoke moja tu ndogo hapo kwenye 'about me'. matokeo yae ndio haya. kweli, ndesyanjo bado ana kazi.......!!
2 comments:
Usijali Chesi,
Utafika tu..sote tulitokea huko.Ukiangalia vizuri kwenye blogu yako utaona kijisehemu chenye kutoa msaada wa kiufundi.Unaweza tumia njia hiyo kujifunza mengi juu ya tekinolojia hii.
Chesi hebu kodolea hapa na ufuate maelekezo yake.
http://help.blogger.com/bin/answer.py?answer=776
Kisha soma taratibu utaelewa tu kupandisha picha yako. Unatakiwa uwe nayo tayari kama kwenye desktip hivi (ya ukubwa wa kawaida hivi). Anza kama unataka ui-upload kama posting ya kawaida (kama ulivyoanza kuiweka hiyo iliyopo). Ukisha i-upload utakwenda kuibadilisha HTML. Huko utakuta URL (address) ya picha. Icopy URL kama walivyonyesha kwenye mfano wao na ui-paste utakaporudi kwenye 'edit profile' (Baada ya kucopy URL utaghairi kuiupload au unaweza endelea nayo ili u-delete baadaye kabisa)
Utaelewa mwenyewe utakapofuata kuunganishi hicho hapo juu. Soma taratibu na utaelewa tu.
Post a Comment