Thursday, April 20, 2006

chesimpilipili

Ndesanjo, nadhani somo lako kuhusu kublogu limeingia barabara. nakushukuru sana. sasa na tuanze kazi.....

11 comments:

Ndesanjo Macha said...

Chesi watu kama wewe ndio mmekuwa mkisubiriwa huku bloguni. Ni furaha kubwa kuona kuwa umeingia kwenye kijiji chetu hiki. Karibu sana.

John Mwaipopo said...

Chesi hebu karibia ndani haraka maana unaweza kunyakwa na majahili hapo nje halafu ukatokomea mbali. Karibu! karibu! Karibu! Tuwekee na kapicha kako maana tumekusahau na hatujui kile kipara kimeongezeka au la.

mwandani said...

karibu, jina lako nalikumbuka vyema tu

boniphace said...

chesi karibu bwana tutakuwa tunakucheki cheki hivi kabla ya mechi za chesii.Haya kazi kwako

Chesi said...

dah! waungwana nashukuru mno kwa makaribisho yenu. basi namii ngoja kwanza ntafute kijipicha changu halafu nikibandike hapo ili tukizungumza tuwe 'tunaangaliana' uso kwa uso....!

Christian Bwaya said...

Jina lako ni kubwa sana mzee. Ninafurahi kuwa tutakuwa tunapata vitu vyako laivu laivu bila kutegemea magazeti kale. Karibu nyumbani kwetu.

Rama Msangi said...

Jamaa wa Mwananchi wametupiga bao sana, na siku zote nimekuwa nikihangaika kuona nitafanya nini ili 'Makolamunist' wa Majira, wanaingia ulimwengu huu na kuja kwako naamini ni mwanzo tu. Nadhani baada ya muda si mrefu Mlala-Hoi (au anatudanganya huwa analala hai?, naye atakuja dimbani na kaka zangu wengine kina Mapinduzi, Kaguo nk.

Nitaanza kuvimbishiana msuli muda si mrefu na akina Makene na Ndesanjo maana kwa uchache sana hivi sasa tuna Rashid Mkwinda, Yakub Nyembo, Hudson Kazonta, Seif wa Arusha na kimsingi mie mwenyewe na wewe mwenyewe.

Kaibu iwe mghoshi, tibindiize ndima

Jeff Msangi said...

Chesi,
Nakumbuka zamani niliwahi kusoma moja ya makala yako ambayo mpaka leo bado iko kichwani na huwa napenda sana kuwaambia watu juu yake.Ulikuwa umeandika juu ya "Adha ya lifti".Kama inawezekana tafadhali tupandishie tena ile makala.Karibu sana uwanjani..ngoma ndio kwanza zinapashwa moto.

Rashid Mkwinda said...

Du yaani patamu hapo, Umhuuuuf!!!!hivi sasa naweza kupumua angalau,kwa kuingia huyu kingunge ndani ya Blogu, maana nilikuwa najisikia kama vile tuwapweke ndani ya hii blogu watu tunaoandikia gazeti la MAJIRA, wenzetu wa Mwananchi walikuwa wanatupiga bao kichizi, mimi nadhani hivi sasa gazeti Tando litazidi kuwa hai na kuimarika zaidi. lakini kabla hujapandisha picha yako tafakari kwanza kwani humu ndani watu wanabonda bila kuangalia huyu ni Kiongozi wa nchi ama ni Waziri,ingawa kuna Azimio la Dom limeanza kuimarishwa kulinda maslahi ya Blogu, nahofia wasije wakaanza kukuwinda kunako mitaa na mikahawa, wakakuKolimba, lakini si mbaya kwa kuwa jina lako linajulikana nahisi hata mwenyewe unajulikana ni uamuzi wako kupandisha kijipicha chako ama la.

Si unaona Bw. Michuzi pamoja na yeye kuwa ni 'mpicha piga' maarufu lakini haweki picha yake anaweka za wenzie tu, mie naona hii iwe ni mada ya kuanza kuchangia katika kumkaribisha Mpilipili ndani ya Blogu au vipi?,tujiulize ni kwani huyu Michuzi hataki kupandisha picha yake ndani ya Blogu ilhali anapandisha za wenzie tu?

Wakatabahu

Chesi said...

jamani asanteni kwa mikaribisho rundo. Mkwinda una hoja kuhusu Michuzi kutoweka kapicha kake kwenye eneo lake la kujida. lakini nakumbuka kuona picha yake moja ameshika bonge la glasi ya chinywaji na nikamuuliza iwapo hiyo sehemu aliyokuwepo ilikuwa haina glasi za saizi ndogo. hajajibu.

Vempin Media Tanzania said...

Karibu sana Mpilipili umwage pilipili ndani ya blogu ee bwana ee nimepata kukusoma wakati ukiwa katika Nipashe hivi sasa huwa nakusoma ukiwa ndani ya Majira karibu sana mzee utubandikie na taswira yako.